Connect with us

Soka

Yanga yanasa kitasa cha KMKM

Mabingwa wa kihistoria nchini Yanga sc imemsajili na kumtambulisha mlinzi wa kati wa mabingwa wa Zanzibar KMKM Ibrahim Bacca kwa mkataba wa miaka miwili kukipiga Jangwani.

Kitasa huyo alikuwa kwenye kiwango bora katika mashindano ya kombe la Mapinduzi yaliyomalizika hiyo jana na alifanikiwa kuwadhibiti vyema washambuliaji wa Yanga wakiongozwa na Makambo wtimu hizo zilizokutana kwenye hatua ya makundi.

Bacca ni aina ya mabeki wa kisasa wenye utulivu mguuni na uwezo mkubwa wa kupiga pasi na kuzuia washambuliaji waumbufu kitu ambacho kimewavutia mabosi wa Yanga kumvalisha uzi wa kijani na njano.

Beki huyo ataenda kuisaidia Yanga kwenye idara ya ulinzi ambayo imekuwa ikikubwa na majeruhi mengi siku za hivi karibuni,ambapo mabeki Kibwana Shomari na Abdallah Shaibu watakosekana kwa muda baada ya kupelekwa Tunisia kwa matibabu hivyo kusababisha safu hiyo kupungukiwa watu muhimu mkwenye eneo hilo.

Usajili huo wa Bacca ni muendelezo wa utamaduni wa klabu hiyo kusajili wachezaji kutoka Zanzibar na wamekuwa wakifanikiwa kwa kiasi kikubwa.Wachezaji kama Nadir Haroub,Abdi Kassim,Abdallah Shaibu na Feisal Salum ni miongoni mwa hao ambao wameibeba Yanga kwa kiasi kikubwa na kuifanya klabu hiyo iendelee kuwaamini wachezaji kutoka visiwani humo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka