Connect with us

Soka

Yanga Yaibamiza Mwadui

Klabu ya Yanga sc imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mwadui Fc mchezo wa Ligi Kuu nchini Tanzania bara uliochezwa katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Bao la Yanga lilifungwa dakika ya 6 na Balama Mapinduzi kufuatia shambulizi la kushtukiza lililoanzia kwa Haruna Niyonzima kisha Jafar Mohamed aliyepiga krosi ambapo Ditram Nchimbi alikosa goli baada ya Kipa kucheza kisha mpira kumkuta Mfungaji.

Bao hilo limeweka rekodi ya kuwa bao la kwanza nchini katika mashindano rasmi tangu ligi isimamishwe siku 95 zilizopita kufuatia kusambaa kwa Virusi vya ugonjwa wa homa ya Mapafu (Covid-19).

Ushindi huo Yanga imesaalia nafasi ya tatu ikiwa na pointi 54 sawa na klabu ya Azam fc japo wanatofautiana kwa tofauti ya mabao ya kushinda na kufungwa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka