Connect with us

Soka

Yanga Sc Yatoboa Caf

Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) wametoa orodha mpya kwenye maeneo yanayoshindaniwa kwenye tuzo za vilabu, wachezaji, makocha na timu za Taifa ambao wamefanya vizuri katika michuano iliyochini ya shirikisho hilo barani Afrika.

Katika orodha baada ya mchujo Timu ya Taifa ya Tanzania ambayo ilikuwa inashindania timu bora imeondoshwa kama ilivyo kwa mlinda mlango wa Yanga Djigui Diarra ambaye alikuwa anagombea kipa bora naye ameondolewa.

Klabu ya Yanga yenyewe imefanikiwa kuingia  5 bora katika kugombea klabu bora ya msimu ambapo sasa itashindana na klabu za Mamelod Sundowns,Al Ahly Fc,Usm Algers na Wydad Athletics Club.

Katika orodha ya makipa bora waliobakia ni Ronwen Willliams, Andre Onana, Edou Mendy, Yaccine Bonou na Mohamed ELshanawy.

Ikumbukwe kuwa mchakato wake sio wa kupiga kura kwa links  bali kuna Kamati maalum ya CAF na makundi maalum kama vile klabu shiriki kwenye kalenda ya mashindano ya CAF kwa mwaka husika, bila kusahau Waandishi wa habari waliochaguliwa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka