Connect with us

Makala

Yanga sc Yapata Hasara 1bn

Klabu ya Yanga sc imepata hasara ya bilioni moja katika msimu uliopita wa 2023/2024 kutokana na mapato yake kutokidhi mahitaji na hivyo kuzidiwa na matumizi ya klabu hiyo kwa ujumla.

Akizungumza katika Mkutano mkuu wa klabu hiyo, Mkurugenzi wa Fedha wa Yanga, Sabri Sadick amesema msimu uliopita 2023/24 mapato yalikuwa ni Sh21 bilioni, huku matumizi yakiwa ni Sh22 bilioni ambayo ni sawa na klabu hiyo imeingiza hasara ya Sh1 bilioni.

“Fedha hizo zimetokana na udhamini, kiingilio cha mlangoni, ada za wanachama, zawadi ya ushindi, mauzo ya wachezaji, faida ya mauzo ya jezi na mapato mengine,”Alisema mkurugenzi wa fedha wa klabu hiyo Sabri Sadick.

Katika moja ya eneo lililoonekana kuwa limegharimu pesa ndefu ni mishahara ya mastaa wa klabu hiyo sambamba na benchi la ufundi ambayo imegharimu takribani bilioni 7 huku usajili na uhamisho wa wachezaji ikiwemo kuvunja mikataba ikigharimu bilioni 3 na ushee.

Yanga sc imekua ikisafiri ndani na nje ya nchi kwa ajili ya michezo mbalimbali ya ligi na michuano ya kimataifa ambapo imeonekana kuwa gharama kubwa zaidi zinatumika ambapo zaidi ya bilioni 2.8 zimetumika.

Matumizi ya jumla yanaonekana kufikia bilioni 22.28 huku mapato yakiwa ni bilioni 21.19 na kufanya klabu hiyo kuzidisha zaidi ya bilioni moja katika matumizi ya kawaida ya klabu hiyo.

Msimu ujao bajeti ya klabu hiyo inatarajiwa kuwa bilioni 24 ikiwa ni ongezeko la asilimia kumi kutoka bajeti ya msimu uliopita ambapo fedha hizo zitagharamia mambo mbalimbali kama mishahara,usajili na posho za ushindi kwa mastaa wa klabu hiyo.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala