Connect with us

Soka

Yanga Sc Yapata Bilioni 2 Caf

Klabu ya Yanga imejihakikishia kuvuna Dola 900,000 (zaidi ya TSh2.3 bilioni) kwa kutinga robo fainali Ligi ya mabingwa barani Afrika kwa msimu wa mwaka 2023/2024 ikifuzu kutokea kundi D la michuano hiyo lenye timu za Al Ahly,Medeama Fc na Cr Belouzdad.

Mabingwa hao wa Tanzania wamefuzu hatua hiyo baada ya kuichapa CR Belouizdad mabao 4-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam siku ya Jumapili Februari 25.

Pamoja na kujihakikishia kiasi hicho cha fedha pia endapo Yanga itafanikiwa kutinga nusu fainali ya mashindano hayo itavuna kitita cha TSh3.1 bilioni huku mshindi wa pili akipata TSh5.1 bilioni licha ya kupoteza mchezo wa fainali.

Bingwa wa michuano hiyo atavuna zaidi ya Sh10.2 bilioni kiasi ambacho walipata Al Ahly msimu uliopita baada ya kuichapa Wydad 3-2 kwenye fainali hizo ambapo kwa mujibu wa Caf huchezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.

Yanga imeitangulia Simba ambayo inasubiri mchezo wa mwisho dhidi ya Jwaneng Galax kufuzu robo fainali na kuungana na bingwa mtetezi Al Ahly, Mamelodi Sundowns, TP Mazembe, Petro Luanda na Asec Mimosas.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka