Connect with us

Soka

Yanga sc Yaondoshwa Afrika

Klabu ya Yanga imeondoshwa kwenye kinyang’anyiro Cha klabu bora barani Afrika baada ya mchujo wa mwisho kuzipitisha klabu za Al Ahly, Wydad Casablanca na Mamelodi Sundowns kuwania tuzo hiyo itakayotolewa Disemba 11 jijini Marrakech.

Klabu ya Yanga imeishia kwenye tano bora Africa baada ya majina matatu ya timu zinazowania tuzo ya klabu bora ya Mwaka Afrika kutolewa na CAF mchana wa leo na kuhitimisha rasmi ndoto ya klabu hiyo kuweka rekodi ya kuwa klabu bora ya msimu barani Afrika.

Yanga sc iliingia katika kinyang’anyiro hicho baada ya kufanya vizuri msimu uliopita ambapo ilicheza fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Usm Algers ya nchini Algeria na kukosa kombe baada ya matokeo ya jumla kuwa 2-2 na kuwafanya kukosa kombe kwa bao la ugenini.

Hata hivyo pamoja na kukosa tuzo hiyo Yanga sc wanapaswa kujivuna kutokana na mafanikio ya msimu uliopita ambapo kwa miaka mingi klabu za Tanzania hazijawahi kufika katika hatua hiyo.

Hata hivyo pia msimu huu klabu hiyo imeendelea kuonyesha muelekeo wa kufanya vizuri kutokana na mpaka sasa kuongoza katika msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini huku pia ikifanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika baada ya miaka 25.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka