Connect with us

Makala

Yanga Sc Yaipiga Pamba Jiji 4G

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuchukua alama tatu muhimu katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini dhidi ya Klabu ya Pamba Jiji katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.

Kocha Miguel Gamondi aliamua kuanza na mshambuliaji Jean Baleke akisaidiwa na Stephan Aziz Ki pamoja na Abubakar Salum aliyeanza kama kiungo wa ulinzi akichukua nafasi ya Khalid Aucho huku eneo la ulinzi wakianza Djigui Diarra na mabeki wa kati Dickson Job na Ibrahim Hamad Bacca sambamba na Bakari Mwamnyeto.

Ibrahim Hamad alifunga bao lake la pili katika ligi kuu ya Nbc nchini kwa kichwa akiunganisha kona ya Maxi Nzengeli na kuipa Yanga sc bao la uongozi dakika za mwanzoni mwa mchezo huku mwishoni mwa kipindi cha kwanza Stephen Aziz Ki alifunga kwa penati baada ya Baleke kuangushwa ndani ya eneo la hatari.

Pamba jiji walilazimika kucheza pungufu katikati mwa Kipindi cha kwanza baada ya beki wao wa pembeni Salehe Masoud kupewa kadi nyekundu na kipindi cha pili waliamua kukaa nyuma lakini walifungwa bao la tatu na Maxi Nzengeli baada ya mabeki kuzembea kuokoa mpira uliokua unaelekea golini dakika ya 54 ya mchezo.

Mabadiliko ya kumuingiza Cletous Chama na Kennedy Musonda yaliwalipa Yanga sc baada ya Musonda kufunga bao la nne kwa Yanga sc dakika ya 85 ya mchezo.

Yanga sc baada ya ushindi huo imefikisha alama 12 ikiwa katika nafasi ya nne ya msimamo wa ligi kuu huku Pamba Jiji ikiwa katika nafasi mbaya ya pili kutoka mkiani ikiwa na alama nne katika michezo saba ya ligi kuu ya Nbc ambapo haijapata ushindi wa aina yeyote mpaka sasa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala