Connect with us

Soka

Yanga sc Wakatisha Kambi Morroco

Klabu ya Yanga sc imekatisha ratiba ya kambi ya maandalizi kujiandaa na michuano mbalimbali inayoendelea nchini Morroco kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuitwa kwa baadhi ya mastaa kujiunga na timu zao za Taifa.

Mpango huo wa kusitisha kambi umetangazwa na kaimu mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo Eng.Hersi Said ambapo sassa italazimika mastaa wa timu hiyo kurejea nchini haraka kuendelea na mazoezi kwa siku kadhaa zilizosalia kabla ya kufika kilele cha siu ya mwananchi kinachofanyika siku ya jumapili Septemba 29 jijini Dar es salaam.

Yanga sc ina kazi kubwa ya kutafuta muunganiko wa timu kufuatia kusajili mastaa wapya kikosini wakiwemo mastaa wa kimataifa ambao pia wanahitaji kuzoea mazingira ya hali ya hewa nchinin ili kuleta ufanisi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka