Rais wa Yanga SC Hersi Said pamoja na Kamati yake ya Utendaji wamekubaliana kuwa mechi yao dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini siku ya Jumamosi ya March 30, 2024 itakuwa bure sehemu za mzunguko ili kufanikisha kujaza mashabiki wengi zaidi uwanjani siku hiyo.
Hayo yamesemwa na Ali Kamwe ambaye ni Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo katika mkutano na waandishi wa habari mchana wa leo uliofanyika katika makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Twiga na Jangwani huku wakitangaza gharama zao za tiketi zitakuwa VIP A Tsh 30,000, VIP B Tsh 20,000 na VIP C Tsh 10,000.
“Wote tunakubaliana mechi ya Mamelodi ni mechi kubwa zaidi kwenye robo fainali ya CAFCL msimu huu na Viingilio ni kama vifuatavyo πππ π ππ,πππ,πππ π ππ,πππ,πππ π ππ,πππ na tunafahamu mechi itaisha usiku sana, kwa kuwajali mashabiki wetu na dhamira ya nchi yetu hasa kwenye sekta ya michezo Viongozi wetu wameamua jukwaa la mzunguko litakuwa bure”
Pia Kamwe ametoa taarifa kuhusu hali za wachezaji ambao ni majeruhi ambapo amesema kuwa mlinzi wa kulia wa klabu hiyo Yao Kouasi alipata majeraha ya nyama za paja katika mchezo wa Ligi kuu dhidi ya Azam FC,ambapo mpaka sasaΒ bado hali yake ni 50/50 ya kuwahi mchezo huo.
Kiungo Khalid Aucho anaendelea kuimarika ambapo naye ripoti ya Daktari itatoa majibu muda si mrefu huku upande wa Kibwana Shomari ambaye anasumbuliwa na enka yeye ataanza rasmi mazoezi siku ya jumatatu.
Yanga sc itakua na kazi ngumu katika mchezo huo kuhakikisha inapata ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo makubwa kwa ngazi za vilabu barani Afrika.