Connect with us

Makala

Yanga Sc Ubabe Ubabe

Yanga sc imeendeleza Ubabe kwa Simba sc baada ya kuifunga 1-0 na kufanikiwa kuingia Fainali ya kombe la Ngao ya jamii katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Simba sc licha ya kuwa na kikosi kisichokua na muunganiko iliamua kupishana na Yanga sc dakika zote tisini za mchezo huo uliokua na kasi ya kutosha huku kukiwa na kosakosa kadhaa ikiwemo za mapema kutoka kwa Shomari Kapombe na Prince Dube.

Bao pekee katika mchezo huo lilifungwa na Maxi Nzengeli dakika ya 44 ya mchezo kwa shuti kali akimalizia pasi nzuri ya kugongeana baina ya Prince Dube na Pacome Zouzoua.

Kipindi cha pili mchezo uliendelea kuwa na kasi lakini Simba sc walikosa ubunifu mbele ya lango licha ya kusaidiwa na kasi ya Joshua Mutale.

Mwamuzi Henry Sasii na wasaidizi wake waliingia matatani kwa kukataa penati za Azizi Ki na Kelvin Kijiri huku pia wakikataa bao la wazi la Azizi ki wakisema kuwa alikua ameotea.

Yanga sc sasa itakutana na Azam Fc katika mchezo wa fainali siku ya Jumapili katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala