Connect with us

Soka

Yanga sc kuwakosa maproo watatu CAF

Klabu ya soka ya Yanga inaweza kuwakosa wachezaji wake watatu wakimataifa katika hatua ya awali ya mtoano klabu bingwa Afrika dhidi ya Rivers United ya Nigeria kutokana na kuchelewa kutolewa kwa ITC za wachezaji hao kutoka vilabu walivyokuwa wakivichezea.

Wachezaji hao ni kiungo Mganda Halid Aucho na Wakongomani wawili beki Djuma Shabani na mshambuliaji Fiston Mayele.

Kukosekana kwa wachezaji hao ni pigo kwa Yanga katika harakati zao za kufuzu makundi ya klabu bingwa Afrika ambayo ndiyo malengo yao kutokana na uzoefu na uwezo wa waachezaji hao katika michuano hiyo.

Katika hatua nyingine Yanga wametambulisha kauli mbiu yao kuelekea michezo hiyo ambayo ni ”The Returns of Champions” wakimaanisha kurejea kwa mabingwa katika kutia hamasa mashabiki na wachezaji wao kufikia malengo,amesema msemaji wa klabu hiyo Haji Manara.

Manara pia amesema kuwa mpaka sasa hawajapewa taarifa yoyoye kama mashabiki wataruhusiwa katika mchezo wa nyumbani dhidi ya Rivers United Jumapili hii kwa Mkapa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka