Connect with us

Soka

Yanga sc Kuhamia Kwa Mkapa

Kuelekea mchezo wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Kocha Mkuu wa Yanga, Nasraddine Mohammed Nabi ametaka kufanya mazoezi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa siku za Ijumaa na Jumamosi.

Siku ya Jumapili 12 septemba inafahamika Yanga wataliwakishirisha Taifa watakapowakaribisha Rivers United ya Nigeria, mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa huku marudiano yakifanyika baada ya siku saba nchini Nigeria.

Afisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, amesema Kocha Nabi amependekeza mazoezi yawe kwa Mkapa ili kutoa nafasi ya kuuzoea uwanja huo mapema hasa kwa wachezaji wa kigeni waliosajiliwa msimu huu.

“Ukizingatia kikosi chetu kina wachezaji wapya, ambao kimsingi wanapaswa kupata nafasi ya kuujua uwanja, wengine wamefika mara moja tu, hivyo kuna umuhimu sana kupata fursa ya kuutumia kabla ya mchezo wenyewe,” amesema Bumbuli.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka