Connect with us

Soka

Yanga Sc Kileleni na 5G

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kusimama kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini baada ya kuifunga Ihefu Fc kwa mabao 5-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Chamazi Jijini Dar es salaam jioni ya leo Jumatatu ya Machi 10 2024.

Yanga sc ilianza kupata bao la mapema dakika ya tisa ya mchezo kupitia kwa Pacome Zouzoua kufutia pasi nzuri ya Azizi Ki katika eneo la hatari ya klabu ya Ihefu Fc huku Mudathiri Yahya tena akimalizia kazi nzuri aliyoianzisha dakika ya 30 baada ya kumalizia pasi nzuri ya Azizi Ki huku Ki mwenyewe akifunga bao la tatu akipokea pasi ya Pacome dakikaya 68 ya mchezo huo.

Azizi Ki akiwa katika ubora wake alitoa pasi nzuri kwa Augustine Okrah aliyefunga bao la nne dakika ya 84 ya mchezo huku Maxi Nzengeli akifunga bao la tano kwa Yanga sc dakika moja baadae baada ya mpira kugonga mwamba wa juu na kurudi uwanjani huku Mwamuzi akiamuru kuwa goli.

Yanga sc kutokana na ushindi huo sasa imezidi kujichimbia kileleni ikiwa na alama 49 katika michezo 18 ya ligi kuu huku Azam Fc ikiwa na alama 44 katika michezo 20 ya ligi kuu ya Nbc nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka