Connect with us

Soka

Yanga Sc Kamli Gado Algeria

Kikosi cha wachezaji wa klabu ya Yanga sc kimekamilika nchini Algeria kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika hatua ya makundi dhidi ya CR Belouzdad utakaofanyika siku ya kesho ijumaa nchini humo.

Awali mastaa wa kikosi hiko waliondoka kwa mafungu ambapo wale waliokua na Timu ya Taifa ya Tanzania waliachwa nchini huku wengine wakitarajiwa kuungana na timu juu kwa juu.

Wale wa Taifa Stars wakiongozwa na nahodha Bakari Mwamnyeto,Ibrahim Bacca,Dickson Job,Nickson Kibabage,Metacha Mnata,Clement Mzize na AbuuTwalib Mshery waliondoka alfajiri ya jumatano Novemba 22 na kuwasili mapema asubuhi ya leo huku wakina Aziz Ki,Djigui Diarra na Khalid Aucho wenyewe wamewasili mapema leo kuungana na timu wakitokea katika majukumu ya timu zao za Taifa.

“Kikosi chetu chote sasa kiko hapa Algeria” maneno ya Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe akizungumzia hali ya kikosi cha timu hiyo huku akidhibitisha kufika kwa wachezaji waliokua katika timu zao za Taifa.

Yanga sc kesho Novemba 24 rasmi itaanza mbio za kuwania kufuzu hatua ya robo fainali baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka