Connect with us

Soka

Yanga Sc Kamili Gado

Kuelekea mchezo wa hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika kikosi kamili cha Yanga sc kimeshiriki mazoezi ya jana jioni machi 28 kujiandaa na mchezo huo wa kwanza utakaofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Mastaa waliokua timu za Taifa Djigui Diarra,Kennedy Musonda,Pacome Zouzoua,Stephane Aziz Ki na Bakari Mwamnyeto,Aboutwalib Mshery tayari wameungana na kikosi hicho baada ya wale wa awali Mudathir Yahya,Ibrahim Hamad na Clement Mzize kuwasili nchini mapema zaidi.

Furaha zaidi kwa mashabiki wa Yanga sc ni urejeo wa mapema wa Khalid Aucho aliyekua majeruhi baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa goti sambamba na Zawadi Mauya,Kibwana Shomari ambao walikua majeruhi wa enka ambao tayari wameanza mazoezi.

Beki Yao Kouasi ndiye pekee ambaye mpaka sasa madaktari wanapambana kuona namna ya kumuwahisha kuuwahi mchezo huo na kama ikishindikana basi atakuwepo katika mchezo wa pili nchini Afrika ya kusini.

Yanga sc katika mchezo wa kesho wanapaswa kushinda ili kujiwekea mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya nusu fainali katika mchezo wa marudiano utakaofanyika April 5 nchini Afrika kusini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka