Connect with us

Makala

Yanga Sc Inatia huruma Cafcl

Ni huruma ukiutazama mwenendo wa klabu ya Yanga sc katika michuano ya kimataifa ya klabu bingwa barani Afrika baada ya kukubali kipigo cha pili cha mabao 2-0 kutoka kwa Mc Algers katika mchezo uliofanyika Jumamosi usiku jijini Algers.

Yanga sc ambayo sasa inashika mkia katika kundi A awali ilikubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Al Hilal Fc ikiwa nyumbani ambapo pia sasa imepoteza mchezo wa pili kwa kipigo hicho hicho.

Kocha Sead Ramovic aliamua kuanza na kikosi akimpa nafasi Kennedy Musonda kama mshambuliaji akisaidiwa na viungo Pacome Zouzoua na Stephan Aziz Ki huku Mudathir Yahaya,Maxi Nzengeli na Duke Abuya wakiwa eneo la kiungo cha ukabaji huku Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Hamad Bacca sambamba na Tao Kouasi Attouhoula na Nickson Kibabage huku golini akianza kipa Djigui Diarra.

Yanga sc pamoja na kikosi hicho imemaliza mechi hiyo ikiruhusu mabao 2 ya kipindi cha pili kutokana na makosa ya safu ya ulinzi.

Mabao ya Ayoub Abdellahoui dakika ya 64 kwa kichwa na lile la dakika ya 90+5 lililofungwa na Soufiane Bayazid na kuwaweka wananchi katika hatari kutofuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Sasa Yanga sc wanapaswa kushinda michezo yake minne iliyosalia ya kundi A ikianza na mchezo ujao dhidi ya Tp Mazembe utakaofanyika ugenini Lubumbashi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala