Connect with us

Soka

XAVI atambulishwa rasmi Camp Nou

Klabu ya Fc Barcelona imemtambulisha kocha wao mpya Xavi Hernandes katika uwanja wa Nou Camp Jijini Barcelona katika tukio lililohudhuriwa na mashabiki na wanachama wengi wa klabu hiyo.

Tukio hilo liliendana na kusaini mkataba wa kazi pamoja na kuwasalmia mashabiki waliofurika uwanjani hapo.

Xavi amesema kuwa Barcelona ni klabu kubwa duniani hivyo wana kazi kubwa ya kufanya kuirudisha kwenye ubora wao hivyo yeye na benchi lake la ufundi wamejipanga vya kutosha kuhakikisha heshima ya klabu hiyo inarudi pamoja na kurejesha soka la kuvutia.

Kiungo huyo wa zamani wa Hispania amesaini mkataba hadi 2024 na amesema kuwa ana furaha kurejea mahali ambako yeye anapaita nyumbani.

Mashabiki wa klabu hiyo waliohudhuria uwanjani hapo wameonekana wakishangilia na kuliimba jina lake na kuonesha imani kubwa kwa nahodha huyo wa zamani wa timu hiyo katika kuijenga Barcelona mpya.

Xavi ameungana na wachezaji wengine kama Pep Guardiola,Luis Enrique,Ernesto Valverde na Ronald Koeman waliowahi kucheza na kuifundisha klabu hiyo kwa vipindi tofauti tofauti.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka