Connect with us

Soka

Woodward kusalia Man Utd

Mtendaji mkuu wa Manchester United Ed Woodward ataendelea na kushikiria nafasi hiyo hadi pale atakapokamilisha mchakato wa kupata kocha wa muda na baadae kocha wa kudumu ndani ya klabu hiyo.

Mkataba wake ulikuwa unaisha mwishoni mwa mwaka huu lakini wamiliki wanataka abakie akamilishe kwanza zoezi hilo.

Man Utd ilisitisha mkataba wa kocha wake mkuu Ole Gunnar Solskjaer siku ya Jumapili na kumpa majukumu ya kukaimu nafsi hiyo Michael Carrick ambaye alikua kocha msaidizi.

Majina kama Laurent Blanc,Carrick mwenyewe,Ralf Rangnick wanatajwa kuwania nafasi ya kocha wa muda mpaka mwishoni mwa msimu huu huku Mauricio Pochettino,Zinedine Zidane na Eric Ten Haag wakitajwa kuchukua majukumu ya kocha mkuu msimu utakapotamatika.

Hata Pochettino ndiye chaguo la kwanza la bodi ya Manchester United kuchukua mikoba ya Ole,huku kocha huyo wa sasa wa PSG akionesha nia ya kurejea Uingereza.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka