Connect with us

Soka

Winga Teleza Wa As Vita Kutua Yanga

Baada ya usajili wa Bernard Morrison aliyetokea DC Motema Pembe ‘kubamba’, inaelezwa Yanga inamnyemelea mchezaji kutoka klabu ya AS Vita ya huko DR Congo.

Winga Tuisila Kisinda ndiye anayetajwa kutakiwa na mabingwa hao wa kihistoria ukiwa ni mkakati wa kuisuka upya Yanga ya mataji.

Nyota huyo ni miongoni mwa waliopendekezwa na kocha Luc Eymaael katika kuimarisha safu yake ya ushambuliaji.

Kisinda ni mmoja wa wachezaji mahiri wa klabu ya AS Vita. Nyota huyo pia anamudu kucheza nafasi ya mshambuliaji wa kati.

GSM ndio inayoipa jeuri Yanga wakati huu, inaelezwa wametenga kitita cha Tsh Bilioni 1.5 kwa ajili ya usajili huku nyota wanne wa kigeni watasajiliwa ambapo Eymael tayari amewasilisha mapendekezo yake.

Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema katika usajili ujao wako tayari kutumia hata dola laki tano kumnasa mchezaji yeyote aliyependekezwa na Eymael.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka