Connect with us

Soka

Waziri Ndumbaro Akutana na Simba Sc,Yanga Sc

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi Kuu (TPBL) na wawakilishi kutoka Klabu za Simba na Yanga ili kujadili masuala mbalimbali kuhusu maendeleo ya michezo hapa nchini na kuweka mikakati ya Klabu za Simba sc na Yanga sc zinazoshiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika zifanye vizuri katika michuano hiyo.


Akizungumza na viongozi hao leo Machi 20, 2024 Jijini Dar es Salaam Mhe. Ndumbaro ameendelea kusisitiza uzalendo akiwaomba Watanzania waendelee kuziunga mkono Yanga na Simba kuelekea kwenye mechi zao za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufanya hamasa na kufika kwa wingi Uwanja wa Benjamin Mkapa kuzishangilia Machi 29 na 30 mwaka huu.

“Tumeziambia timu zote mbili zishirikiane na Serikali katika kipindi hiki ili kupata mafanikio kwa hiyo timu mbili zitakwenda kujipanga watasema wanahitaji Serikali ifanye nini ili kuhakikisha timu zinafanya vizuri kwa upande wa Serikali tuko tayari, uwanja uko tayari, masuala yote ya kiusalama yako tayari, maandalizi ya tiketi yako tayari na masuala mengine ambayo ni muhimu kwa Serikali kuyafanya ili mechi hizo ziwe kufanyika vizuri “amesisitiza Dkt. Damas Ndumbaro

Mhe. Ndumbaro ameeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuonesha utayari mkubwa kwenye michezo wakati huu ambao Watanzania wanasherehekea mafanikio ya miaka mitatu ya uongozi wake akibainisha kuwa kwenye mashindano ya Kimataifa ameongeza hamasa kwa wachezaji. “Mhe.Rais alikuwa anatoa shilingi milioni tano kwa goli sasa anatoa Milioni 10 kwa kila goli, mnaona kabisa mama yetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongeza dau hilo ili timu zetu mbili ziweze kufanya vizuri na zipate mafanikio zaidi” ameeleza Dkt. Damas Ndumbaro

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Klabu ya Simba ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Imani Kajula amesema watahakisha mara zote wanaweka nchi mbele katika michuano hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka