Connect with us

Soka

Wawili Simba sc Kuikosa Ruvu Shooting

Klabu ya Simba sc leo itacheza mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Ruvu Shooting mchezo utakoafanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam huku ikwakosa mastaa kadhaa katika mchezo huo.

Jonas Mkude na Eldin Sharaff Shiboub wataukosa mchezo huo baada ya Mkude kuwa majeruhi ambapo aliumia katika mchezo dhidi ya Kmc katika uwanja wa Mo simba arena na atakaa nje kwa wiki mbili huku Shiboub yeye akiwa bado hajawasili kutokana na changamoto ya Virusi vya Corona ambapo nchi ya Sudan imefunga mipaka yake.

Pia Cletous Chama na Miraji Athuman nafasi zao zipo katika hatihati kufuatia kutokua fiti kutokana na sababu mbalimbali wakati Chama alichelewa kujiunga na timu huku Miraji akitokea majeruhi ya muda mrefu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka