Connect with us

Soka

WATATU WATAJWA KUMRITHI SMITH ASTON VILLA

Makocha watatu wapo kwenye orodha ya klabu ya Aston Villa kuchukua mikoba ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Dean Smith aliyefutwa kazi siku ya Jumamosi baada kupoteza michezo mitano mfululizo ya ligi kuu.

Kocha wa kwanza ni Roberto Martinez kocha wa timu ya Taifa ya Ubelgiji ambaye hata hivyo itakuwa ngumu kumpata kutokana na kuhitaji kuiongoza Ubelgiji kwenye michuano ya kombe la dunia Qatar 2022.

Steven Gerard wa Rangers ya Scotland ni chaguo lingine kwenye orodha japo naye ni ngumu kuiacha klabu anayofundisha katikati ya msimu wakati huu timu yake ikiongoza msimamo wa ligi kuu ya Scotland.

Chaguo la tatu ni kocha wa sasa wa Southampton Ralph Hasenhult ambayo ndiye anayeweza kupatikana kulingana na udogo wa Southampton katika dirisha la usajili na nia ya kocha huyo kutaka kujitanua zaidi kwa kwenda kwenye timu yenye misuli zaidi.

Aston Villa haijafanya vizuri tangu kuondoka kwa nahodha wake Jack Grealish aliyejiunga na Manchester city kwa dau lililovunja rekodi ya usajili kwenye ligi kuu soka nchini Uingereza.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka