Connect with us

Soka

Waamuzi Sita Kuamua Yanga vs Simba

Bodi ya ligi nchini TPLB imetangaza rasmi kuwa mchezo wa ligi kuu nchini baina ya Yanga sc dhidi ya Simba sc utachezeshwa na waamuzi sita ili kuleta ufanisi zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa Benjamini Mkapa katika mkutano maalumu na wanahabari mtendaji mkuu wa TPLB Almas Kazongo alisema kuwa wao kama wasimamizi wa mchezo huo wameona inafaa kutumia waamuzi sita ambapo wanne watakua kama ilivyo mechi zingine huku wale wawili watakaoongezeka watakua nyuma ya magoli.

Mchezo huo wa kusisimua unatarajiwa kufanyika Novemba 7 siku ya jumamosi katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam ambapo katika mchezo wa mwisho timu hizo kukutana Yanga alifungwa mabao 4-0.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka