Connect with us

Soka

Gwambina Wabishi Hao

Licha ya jitihada za klabu ya Yanga sc kutaka kuibuka na alama zote tisa kanda ya ziwa lakini juhudi na kujitoa kwa wachezaji wa Gwambina zimesababisha matokeo ya suluhu katika mchezo uliofanyika jioni hii katika uwanja wa Gwambina Complex Misungi jijini Mwanza.

Yanga iliyowapumzisha mastaa wake karibuni wote ilianza mchezo taratibu na kusababisha kushambuliwa mara kwa mara huku mwamuzi akikataa bao la Jacob Massawe ambaye aliuvunja mtego wa kuotea na mpaka mapumziko timu hizo zilikua hazijafungana.

Kuingia kwa Michael Sarpong kulibadili mchezo kipindi cha pili na kupelekea Yanga kutawala japo mpaka mpira unamalizika hakuna timu iliyopata bao.

Yanga wanapanda mpaka nafasi ya kwanza wakiwa na alama 23 huku Azam wakiwa katika nafasi ya pili na alama 22.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka