Connect with us

Soka

Valverde kwenye rada za Man Utd

Klabu ya soka ya Manchester united ya Uingereza imefanya imewasiliana na mkufunzi wa zamani wa Fc Barcelona Ernesto Valverde kuhusu nafasi ya kuwa kocha wa muda wa timu hiyo.

Man Utd kwasasa inatafuta kocha atakaehudumu Old Trafford hadi mwishoni mwa msimu huu itakapokamilisha mchakato wa kupata kocha mkuu mpya baada ya kufukuzwa kwa Ole.

Bodi ya timu hiyo inamuona kocha wa sasa wa PSG Mauricio Pochettino kama chaguo la kwanza kwenye nafasi ya kocha mkuu,na endapo watafanikiwa kumpata kwa wakati huu basi wataachana na mpango wa kutafuta kocha wa muda.

Katika mkutano na waandishi wa habari hapo jana kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya Man City,Pochettino alisema ana furaha kuwa PSG,analipenda Jiji la Paris na mashabiki wake,hata hivyo kocha huyo anatajwa kutokuwa na furaha na maisha ndani ya miamba hiyo ya Ufaransa na yupo tayari kuondoka.

Valverde alifukuzwa kazi Barca mwaka 2018,lakini uwezo wake wa kuzungumza Kiingereza ndio unaotajwa kufikiriwa na mabosi wa United.Kocha huyo ni mshindi kwani alitwaa mataji mawili ya ligi akiwa na Olympiacos ya Ugiriki na Fc Barcelona.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka