Connect with us

Soka

Ujerumani ya kwanza kufuzu Qatar 2022

Timu ya Taifa ya Ujerumani imekuwa ya kwanza kufuzu michuano ya kombe la dunia 2022 nchini Qatar baada ya ushindi mnono wa magoli 4-0 ugenini dhidi ya Macedonia ya Kaskazini usiku wa kuamkia leo kwenye kundi J ukanda wa Ulaya.

Mabao mawili kutoka kwa Timo Werner na mengine ya Jamal Musiala na Kai Havertz yalitosha kuhakikisha Ujerumani inakata tiketi hiyo muhimu kwa kocha mpya wa timu hiyo Hans Flick aliyechukua mikoba ya Joachim Low.

Ujerumani haikuwa katika kipindi cha mwisho chakocha Joachim Low,hivyo ujio wa Hans Flick na maingizo ya damu changa kumetoa matumaini kwa Wajerumani kufanya vizuri katika michuano ya kombe la dunia mwakani.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka