Connect with us

Soka

Ufaransa bingwa ligi ya mataifa Ulaya

Timu ya Taifa ya Ufaransa imetwaa ubingwa wa ligi ya Mataifa Ulaya 2021 kwa kuwafunga timu ya Taifa ya Hispania kwa mabao 2-1 katika mchezo wa fainali ulifanyika katika dimba la San Sirro Jijini Milan Italia.

Hispania walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 64 kupitia kwa Mikel Oyarzabal,dakika mbili baadae Ufaransa wallisawazisha kupitia Karim Benzema kabla ya mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe kuipatia bao la ushindi timu yake dakika ya 80.

Mabingwa hao watetezi wa kombe la dunia wametawazwa kuwa mabingwa wapya wa michuano hiyo iliyofanyika kwa mara pili baada ya Ureno kuwa kwanza kuutwaa ubingwa huo mwaka 2019 na linakuwa taji la pili kwa kocha mkuu wa timu hiyo Didier Deschamps.

Nahodha na kiungo wa timu ya Taifa ya Hispania Sergio Busquet amekuwa mchezaji bora wa michuano hiyo katika hatua ya nne bora.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka