Connect with us

Soka

Uchebe Asimamishwa Simba

Timu ya Simba sc imemsimamisha kazi kocha mkuu Patrick Aussems mpaka Novemba 28 mwezi huu ambapo kikao cha bodi ya wakurugenzi kitakapokaa na kutoa maamuzi.

Kwa mujibu wa ripoti za ndani zinadai chanzo cha kusimamishwa kazi kocha huyo ni kutokana na kutohudhuria kikao cha kujieleza baada ya kuwa amesafiri ghafla kwenda nje ya nchi alikodai ana matatizo binafsi.

Uongozi wa Simba ulichukizwa na kutohudhuria kwa kocha huyo katika kikao hicho kilichopangwa kufanyika katika ofisi ya mtendaji mkuu wa klabu hiyo Senzo Masingisa zilizopo katikati ya jiji bila ya kutoa taarifa zozote.

Aussems amethibitisha kupokea barua hiyo huku akisema anawasiliana na wanasheria wake waliopo ulaya ili kujua nini cha kufanya.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka