Connect with us

Soka

K’njaro Queens Yapoteza

Timu ya taifa ya wanawake nchini(Kilimanjaro queens) imeshindwa kutetea ubingwa wa kombe la Chalenji baada ya jana kufungwa mchezo wa fainali kwa mabao 2-0 na Kenya katika uwanja wa chamazi jijini Dar es salaam.

Jentrix Shikangwa aliyeingia kipindi cha pili ndiye aliyeleta kilio kwa Tanzania baada ya kufunga mabao mawili dakika ya 70 kwa penati baada ya beki wa kilimanjaro queens kuunawa huku akifunga bao la pili dakika ya 87 kwa shuti kali akipokea pasi ya Mwanalima Jereko.

Licha ya kutwaa kombe pia Kenya imetoa golikipa bora,mshambuliaji bora huku Tanzania ikitoa mchezaji bora na timu yenye nidhamu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka