Connect with us

Soka

Thiago Silva Anukia Epl

Thiago Silva amesema yu tayari kusalia katika mojawapo ya klabu za bara Ulaya kwa misimu miwili zaidi baada ya waajiri wake Paris Saint-Germain (PSG) kumweleza kwamba hawatarefusha mkataba wake mwishoni mwa muhula huu.

Psg kupitia kwa mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Leonardo walithibitisha kuwa hawatamuongeza mkataba nahodha huyo wa muda mrefu klabuni hapo.

Taarifa za awali zinadai kwamba klabu ya Arsenal ipo mbioni kumsajili staa huyu mwenye miaka 35 japo watakumbana na upinzani mkali kutoka Ac Milan,Everton,Wolves na Westham huku pia timu za kutoka Marekani,Qatar na Brazil zinammndea staa huyo.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka