Connect with us

Makala

TFF Yakwepa Msala wa Lawi

Kamati ya sheria na hadhi za wachezaji ya Shirikisho la soka nchini (TFF) imewapa maagizo klabu ya simba na Coastal union wakae mezani wajadiliane wenyewe wapate hatima kuhusu mchezaji beki lawi ambaye alisaini simba sc huku coastal union nao wakidai baado ni mchezaji wao.

Simba sc na Coastal Union zimeingia katika mgogoro kuhusu usajili wa beki huyo baada ya Simba sc kuchelewesha kukamilisha malipo ya usajili wa beki huyo na kusababisha Coastal Union kuamua kisitisha dili hilo baada ya kupata ofa nono kutoka nchini Ubelgiji ambapo waliamua kurejesha pesa za awali zilizokua zimelipwa na Simba Sc.

Simba Sc wanadai kuwa wanastahili kumtumia mchezaji huyo kutokana na kukamilisha makubaliano yote ikiwemo kumsainisha mkataba mchezaji huyo ambapo walipaswa kukamilisha malipo mpaka kufikia Mei 31 2024 lakini Simba sc walikamilisha malipo hayo siku kumi mbele.

Mpaka sasa taarifa za awali zinasema kuwa licha ya mchezaji huyo kutambulishwa na Simba sc bado yupo mikononi mwa Coastal Union na tayari amekwenda nchini Ubelgiji kwa ajili ya kufanya majaribio katika klabu ya K.R.C Genk ya nchini humo.

Baada ya Simba sc kufikisha suala hilo katika kamati hiyo sasa imeamuliwa pande hizo kukutana kwa ajili ya kujadiliana kumaliza suala hilo huku ikiwa haifamiki endapo watashindwa kamati hiyo itaamua kitu gani.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala