Arsenal huenda ikampoteza mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, ambaye anatakiwa na Real Madrid. Raia huyo wa Gabon mwenye miaka 30 anatakiwa na Zinedine Zidane kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa Inter Milan Lautaro Martinez – ambaye anataka kuhama klabu hiyo ya Italia kuenda Barcelona.(Sport – in Spanish)
Winga wa kimataifa wa Ujerumani na Manchester City Leroy Sane, 24, anakaribia kuhamia Bayern Munich kwa kiasi cha £70m.(Mirror)
Kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz, 20, amedokeza kuwa yuko tayari kuhama, huku Liverpool ikiwa ni miongoni mwa vilabu ya Ligi ya Primia inayomtaka. (Sport Bild – in German)
Mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 33, yuko tayari kupunguziwa mshahara ili apate fursa ya kuhamia Inter Milan msimu huu. (Gazzetta dello Sport – in Italian)
Mlinzi wa Manchester United na Argentina Marcos Rojo, 30, anataka kurefusha mkataba wake wa sasa wa mkopo nyumbani kwao Estudiantes kwa sababu amecheza mara moja tu na kujeruhiwa kabla ya ligi kusitishwa katokana na mlipuko wa vurusi vya corona. (Manchester Evening News)
Wababe wa Italia, AC Milan wameamua kuwasilisha ofa ya kumnunua kiungo wa kati wa England Adam Lallana msimu huu. Mkataba wa mchezaji huyo wa zamani wa Southampton, 31, katika klabu ya Liverpool unamalizika mwisho wa Juni. (Mirror)
Arsenal inatarajiwa kamuuza mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre Lacazette mwisho wa msimu, huku Atletico Madrid wakipigiwa upato kumnunua kiungo huyo wa miaka 28. (AS – in Spanish)
Arsenal inakaribia kukamilisha uhamisho wa bure wa mlinzi wa Ufaransa wa miaka 27 Layvin Kurzawa kutoka Paris St-Germain.(Daily Star)
Beki wa Leicester wa Austria Christian Fuchs, 34, bado hajaamua ikiwa atarefusha mkataba wake katika uwanja wa King Power ama ahamie Marekani kujiunga na familia yake. (Daily Mail)
Mlinda mlango wa Liverpool Loris Karius amesema bado anawasiliana na Jurgen Klopp, japo yuko klabu ya Uturuki ya Besiktas, hana uhakika kuhusu hatima yake ya baadae. Mkataba wa Mjerumani huyo wa miaka, 26, Anfield unaendelea hadi 2022. (Sky Sports)