Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anatafakari uwezekano wa kumsajili beki wa kushoto wa Bayern Munich na Austria David Alaba, 28, msimu huu wa joto. (Mirror)

 

Ajenti wa Kevin de Bruyne anasema kiungo huyo wa kati wa Ubelgiji mwenye aliye na umri wa miaka, 29, hataondoka Manchester City, msimu huu hata marufuku ya Ulaya dhidi ya klabu hiyo itaondolewa. (Sporza – in Dutch)

 

Arsenal inataka kusalia na kipa wa Argentina Emiliano Martinez, 27, baada ya kuahirisha mpango wa kumnunua kipa mpya msimu huu wa joto. (Mirror)

 

Real Madrid wako tayari kupokea ofa ya klabu zinataka kumnunua mshambuliaji wa Serbia Luka Jovic, 22. (Marca)

 

Leicester City wanaamini watafanikiwa kumsajili Jovic kwa karibu £31m na kuthibitisha kuwa tayari wamewasiliana na ajenti wake. (Star)

 

Mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund Michael Zorc anasema klabu hiyo ya Ujerumani imetoa orodha ya wachezaji watakaojaza pengo litakaloachwa na na winga wa England Jadon Sancho, 20, endapo ataondoka msimu huo. (Kicker – in German)

 

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ameifahamisha klabu yake kwamba anataka kumsajili mshambuliaji atakayesaidiana na – Sancho ambaye wanamnyatia – pamoja na mshambuliaji wa wa safu ya kati na nyuma msimu huu. (Telegraph – subscription required)

 

Inter Milan inataka kuwasajili beki wa wa kushoto wa Italia Emerson Palmieri, 25, na mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 33, kutoka Chelsea. (Goal)

Kiungo wa kati wa zamani wa Manchester United Roy Keane ameshindwa kuchagua ni nani anastahili kujiunga na klabu hiyo kati ya kipa wa Tottenham na Ufaransa Hugo Lloris, 33, na mshambuliaji wa Korea Kisini Son Heung-min, 28. (Star)

 

Everton inakabiliwa na kibarua kigumu kumpata mlinzi wa Lille na Brazil Gabriel Magalhaes, 22,baada ya kuchelewa kuwasilisha ombi la kutaka kumnunu mchezaji huyo. (Sky Sports)

 

Ajenti wa mchezaji wa Aston Villa Jack Grealish, 24, anasema kwamba kiungo huyo wa kati hajafikia makubaliano ya kujiunga na Manchester United huku klabu hiyo ikimwekea thamani ya £80m. (Metro}

 

Klabu ya Norwich City imeitisha dau la £50m ili kumuuza beki Ben Godfrey, 22, huku klabu za Borussia Dortmund na RB Leipzig zikiwa miongoni mwa klabu zinazomwania mchezaji huyo wa timu ya England ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21. (Sky Sports)

 

Juventus imeipatia Chelsea ofa ya wachezaji wawili, ikiwemo mchezaji wa Wales Aaron Ramsey, 29, ili kubadilishana na kiuongo wa kati wa Itali Jorginho, 28. (Express via Tuttosport)

Manchester United inamchunguza beki wa Bournemouth na Uholanzi Nathan Ake, 25, beki wa Aston Villa na England Tyrone Mings, 27 na beki wa AC Milan na Italy Alessio Romagnoli, 25, kama chaguo la kushirikiana na beki wa kati Harry Maguire katika safu ya ulinzi ya kati. (ESPN)

 

RB Leipzig imeziba pengo la mchezaji wao anayeelekea Chelsea Timo Werner, 24, ambaye nafasi yake imechukuliwa na mshambuliaji wa Red Bull Salzburg na mchezaji wa Korea Kusini Hwang Hee-chan, 24. Beki wa Ujerumani Benjamin Henrichs, 23, pia anaelekea kujiunga na klabu hiyo ya Bundesliga kwa mkopo kutoka Monaco (ESPN).