Connect with us

Makala

Ten Hag Afukuzwa Man Utd

Mabosi wa klabu ya Manchester United wamefikia maamuzi magumu ya kuachana na kocha Erick Ten Hag baada ya kudumu nae kwa takribani misimu miwili.

Mabosi hao wameachana na kocha huyo baada timu hiyo kuwa na mwenendo usioridhisha ikitoka kufungwa 2-1 na Westham United siku ya Jumamosi na kuzidi kushuka chini katika msimamo wa ligi kuu ya nchi hiyo.

Mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo Ruud Van Nestrooy ametangazwa kama kocha wa muda wa klabu hiyo huku mabosi wa juu wakiwa kwenye mazungumzo na kocha wa klabu ya Sporting Club ya Ureno Ruben Amorim kuchukua nafasi ya Ten Hag na mpaka sasa kikubwa kilichobaki na kukubaliana masuala ya fidia kwa klabu hiyo.

Van Nestrooy atasimama kama kocha katika mchezo ujao dhidi ya Leicester City na inatarajiwa mapema mwezi novemba Amorim tayari atakua ametua klabuni hapo kama kocha mkuu.

Mabosi wa Man Utd kutokana na mwenendo wa timu hawakuona ugumu kukubali kulipa zaidi ya bilioni 35 za kitanzania kumlipa Ten hag ili kuhitimisha miaka miwili na nusu aliyokaa klabuni hapo huku wakongwe wengi wa soka nchini humo akiwemo Jammie Carragher akisema kuwa klabu hiyo imechelewa kuchukua uamuzi huo kwani ilipaswa kuufanya toka mwezi wa sita wakati wa dirisha kubwa la usajili.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala