Connect with us

Soka

Tambwe Anukia Jangwani

Inasemekana uongozi wa klabu ya Yanga sc upo kwenye mipango ya kumsajili mshambuliaji Amis Tambwe kwa mkataba wa muda mfupi ili kuongeza nguvu katika kikosi cha timu katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo.

ambwe kinara wa mabao wa muda wote kwa wachezaji wa kigeni ligi kuu ya Tanzania, anaweza kurejea kuitumikia Yanga mpaka mwishoni mwa msimu

Yanga inahitaji kuboresha safu yake ya ushambuliaji baada ya kuachana na washambuliaji Sadney Urikhob na Juma Balinya

Wachezaji hao walishindwa kutamba licha ya matarajio makubwa kutoka kwa mashabiki

Msimu uliopita Tambwe aliifungia Yanga mabao nane licha ya kutopata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza mara kwa mara

Hakuna shaka anaweza kuongeza kitu kwenye safu ya ushambuliaji ambayo kwa sasa inamtegemea David Molinga pekee

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka