Connect with us

Soka

Taifa Stars Vs Niger Hapatoshi

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kinaendelea na mazoezi kwa ajili ya michuano ya kimataifa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia mwaka 2026 ambapo sasa itawaaa Nigers na Morocco mwezi huu wa Novemba.

Stars kwanza itakua na kibarua kigumu mbele ya Niger mchezo unaotarajiwa kufanyika novemba 18  2023 kwenye mji wa Marrakech nchini Morocco na mchezo wa pili utakuwa nyumbani katika uwanja wa Benjamin Mkapa  dhidi ya Morocco ambao utachezwa Novemba 21, 2023.

Stars inahitaji alama katika michezo hiyo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu hatua inayofuatia ambapo tayari kocha Adel Amrouche amewaita mastaa mbalimbali ambao wameshajiunga na kambi ya mazoezi ya timu hiyo akiwemo Simon Msuva ambaye ametoa neno kuelekea mchezo huo.

“Kucheza timu ya Taifa ni kitu cha kujivuia, unapoitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ni heshima, tupo hapa kwa ajili ya kupambania taifa letu.”Alisema Msuva

“Niger ni timu ambayo tumeshakutananayo mara mbili kwa siku za hivi karibuni, mara ya mwisho tulichezanao hapa nyumbani na tukawafunga goli 1-0.”Aliendelea kusema

“Tunaamini mechi haitakuwa nyepesi lakini tunaendelea kujiandaa vya kutosha kuipigania nchi yetu, kila mtu anajua umuhimu wa hizi mechi mbili lakini mechi dhidi ya Niger itatupa mwanga kuelekea mechi dhidi ya Morocco.”Alimalizia Msuva ambaye anacheza soka la kulipwa nchini Algeria

Katika kufuzu fainali hizo Stars ipo kundi E na timu ngumu za Drc Congo,Morocco,Niger,Zambia na Eritrea.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka