Connect with us

Soka

Tabora United Yamtambulisha Mfaransa

Klabu ya Tabora United imemtambulisha rasmi kocha mpya, Denis Laurent Goavec raia wa Ufaransa kurithi mikoba ya Goran Copunovic punde tu baada ya makubaliano ya pande mbili kuachana na kocha huyo alijiunga na timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu.

Kocha Denis Laurent Goavec mwenye miaka 66 ya kuzaliwa ametambulishwa kama kocha mpya wa klabu hiyo akiwa na kazi kubwa ya kuitoa timu hiyo mkiani mwa ligi kuu ambapo katika mechi za siku za karibuni kikosi hicho kimekua na matokeo mabovu kiasi cha kushika nafasi ya 13 na pointi 21 ikiwa imecheza mechi 21.

Kocha huyo mwenye leseni ya Shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA Pro Licence) ameshafundisha soka barani Afrika katika klabu za As Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Js Soura ya Algeria na timu ya taifa ya Benin ambapo atakua na kazi ya kuhakikisha timu hiyo haishuki daraja katika michezo tisa ya ligi kuu iliyosalia ambapo pia baada ya mechi hizo mkataba wake utakua umeisha.

Kazi kubwa ya kwanza ya Kocha huyo itaanza Aprili 4, 2024 katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) hatua ya 16 bora dhidi ya Singida Fountain Gate katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo anatakiwa aanze kuleta matunda klabuni hapo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka