Connect with us

Makala

Sure Boy Asaini Yanga sc

Taarifa za ndani zinadai kuwa tayari kiungo Abubakari Salum maarufu kama Sure boy tayari amemalizana na mabosi wa klabu ya Yanga sc huku ikisubiriwa kutangazwa rasmi kwa dili hilo.

Awali msimu uliopita Yanga sc ilikua mbioni kumsajili kiungo huyo sukari lakini dili hilo lilikwama baada ya kutoafikiana dau la usajili kwa mabosi wa klabu hiyo na wale wa Azam Fc ambao walihitaji dau nono kuvunja mkataba wa kiungo huyo mwandamizi klabuni hapo.

Mgogoro ulioibuka baina ya Azam fc na wachezaji waandamizi akiwemo kiungo huyo imepelekea kukamilika kwa dili hilo huku ikidaiwa mchezaji huyo hana tena mpango wa kuendelea na maisha ya chamazi kutokana na kutuhumiwa kuwa mtovu wa nidhamu mara kwa mara.

Inaelezwa kuwa klabu ya Yanga sc inamuangalia Sureboy kama mbadala wa Feisal Salum kikosini humo ambapo kila timu pinzani inapofanikiwa kumdhibiti kiungo huyo basi Yanga sc huzidiwa na kukosa mpango mbadala.

Tayari kiungo huyo amewaambia waajiri wake Azam Fc kuwa hana mpango wa kuendelea kusalia kikosini humo akihitaji kuvunja mkataba ili ajiunge Yanga sc klabu ambayo pia aliichezea baba yake mzazi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala