Connect with us

Soka

Stars,Morroco Hapatoshi B/mkapa

Timu ya Taifa ya soka nchini “Taifa Stars” kesho itakua na kibarua kigumu katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la Dunia kwa kundi E dhidi ya Morroco utakaofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Stars tayari ina alama tatu mkononi baada ya kufanikiwa kumfunga Niger ugenini hivyo wanahitaji kuwafunga Morroco ili kupata alama tatu na kukaa kileleni mwa msimamo wa kundi E huku wakiwaombea Zambia,Niger na Congo Dr wapate matokeo mabaya.

Stars kesho itakua na kazi ya ziada kuwadhibiti Morroco wenye mastaa wakubwa wanaocheza soka barani ulaya kama Nayef Aguerd (West Ham), Sofyan Amrabat (Manchester United), Anass Zaroury (Burnley),Achraf Hakim(PSG),Noussair Mazraoui (FC Bayern Munichen),Youssef En-Nesyri (Sevila) na wengineo

Kwa upande wa Tanzania staa mkubwa ni Mbwana Samata anayecheza soka nchini Ugiriki huku pia kukiwa na Simon Msuva anayecheza timu ya JS Kabylie ya nchini Algeria pamoja na Haji Mnoga na Ben Starkie wanaocheza soka nchini Uingereza.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka