Connect with us

Soka

Stars Yawasili Ivory Coast

Kikosi cha Taifa Stars kimewasili Ivory Coast kwenye mji wa San Pedro tayari kwa mashindano ya michuano ya mataifa ya Afrika (Afcon 2024) yanayotaraji kuanza Januari 13, 2024 nchini humo.

Kikosi hicho kinachojumuisha wachezaji 27 pamoja na wataalamu mbalimbali wakiwemo benchi la ufundi sambamba na madaktri,meneja wa timu na viongozi mbalimbali wamewasili nchini humo na kupokelewa kwa shangwe pamoja na vikundi vya ngoma za asili za Taifa hilo.

Stars imefanikiwa kufuzu michuano hiyo kwa mara ya tatu katika historia ya nchi imepangwa katika kundi F sambamba na timu za Morocco,Congo DRC pamoja na Zambia ambapo jumla ya timu mbili zitafuzu hatua ya robo fainali kutoka kila kundi.

Stars itafungua dimba kwa kuivaa Morocco katika michuano siku ya Januari 17 mchezo ambao utakua wa kwanza kwa kundi F huku Zambia itavaa Congo Drc siku hiyo hiyo.

Katika orodha ya mastaa wa Tanzania waliowasili na kikosi hicho majina maarufu ni Simon Msuva,Mbwana Samata,Feisal Salum,Aishi Manula,Mohamed Hussein,Novatus Dismass,Beno Kakolanya,Dickson Job,Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Hamad Bacca.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka