Connect with us

Makala

Stars Yapoteza Dhidi ya DRC

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imepoteza mchezo wa kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika mwaka 2025 dhidi ya DR Congo baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Kocha Hemed Morocco aliamua kumjaribu kocha Sebastian Desabre kwa kuwaanzisha mastaa mbalimbali wanaoweza kushambulia lakini pamoja na kushambulia sana Stars haikuweza kupata magoli pamoja na kuwa na mastaa mbalimbali.

Kikosi hicho kilianza na 1. Ally Salim 2.Lusajo Mwaikenda 3.Mohammed Hussein 4.Ibrahim Bacca 5.Dickson Job 6.Adolf Mtasingwa 7.Kibu Denis 8.Mudathir Yahaya.9.Mbwana Samatta 10.Feisal Salum 11.Clement Mzize lakini mwishoe ilishuhudiwa Stars ikiondoka kichwa chini.

Kipindi cha kwanza kilimalizika timu hizo zikiwa sare lakini mabadiliko ya kumtoa Mudathir Yahaya na kumuingiza Himid Mao yalifanya Stars izidiwe eneo la kiungo huku presha ya mashambulizi ikipungua na kuwapa nafasi Congo kuanza kupanga mashambulizi.

Meshack Elia aligeuka mwiba mchungu kwa Stars alipofunga mabao mawili ya haraka haraka dakika za 87 na 90+3′ na kuwapa Congo alama tatu muhimu.

“Timu imecheza vizuri kuanzia mpira unaanza mpaka tunafungwa mabao, Tumekosa umakini tu kuna muda tulikuwa tunacheza kama tuko mazoezini yote tutayafanyia kazi ila kifupi Tumecheza vizuri”.Alisema kocha wa Stars Hemed Moroco.

Kwa upande wa Drc walisema kuwa walikua wanamhofia Simon Msuva lakini kutoitwa kwake imekua kama ni nafuu kwao.

“Tulikua tunahofu na Msuva kutokana na kasi yake lakini tulipojua hajaitwa tulishukuru na kuona kuna unafuu wa kushinda”.Alisema Fiston Mayele mchezaji wa Congo.

Kutokana na ushindi huo sasa DR Congo wamefuzu moja kwa moja kupitia kundi H kama kinara baada ya kufikisha alama 12 huku nafasi ya Stars kufuzu ikiwa shakani ambapo sasa atalazimika kushinda michezo ijayo miwili dhidi ya Guinea na Ethiopia.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala