Connect with us

Soka

Stars Yalala 2-0 Kwa Morroco

Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imekubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Morroco katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia litalofanyika mwaka 2026 katika nchi za Marekani,Canada na Mexico.

Katika mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam kocha wa Taifa Stars Adel Amrouche aliwashangaza wengi baada ya kuamua kuanza na kikosi ambacho hakina mastaa kama Mbwana Samata,Aishi Manula,Simon Msuva na Feisal Salum akiwaanza wapya kama kipa Kwesi Kawawa,Chalz Mmombwa huku eneo la ushambuliaji akianza na Kibu Dennis pekee.

Iliwachukua Morroco dakika moja kupata penati ambayo Achraf Hakim alipaisha juu ya lango huku Hakim Ziyech akiiandikia wageni bao la uongozi kwa shuti kali dakika ya 28 lililomshinda kipa Kwesi Kawawa.

Stars walijitahidi kujipanga kusawazisha lakini ubora wa Morroco ulikua wa hali ya juu mno ambapo walikua wakicheza namna wanavyojisikia huku kikosi kizima kikiwa na wachezaji wanaocheza soka barani ulaya.

Lusajo Mwaikenda alijifunga katika harakati za kuokoa dakika ya 56 na kuwafanya wageni kuumaliza mchezo mapema kabisa hasa baada ya kujihakikishia kupata alama tatu muhimu.

Sasa Morroco ndio wapo kileleni mwa Kundi E wakiwa na alama sita huku Zambia,Niger na Tanzania zikiwa na alama tatu kila mmoja.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka