Connect with us

Makala

Songombingo Kagame Cup

Zikiwa zimesalia takribani wiki mbili michuano ya Kagame Cup ianze nchini Tanzania,mpaka sasa timu mwenyeji za Simba Sc,Yanga Sc na Azam Fc ambazo zilitajwa kushiriki michuano hiyo zina mpango wa kutoshiriki kutokanwa na kubanwa na ratiba za maandalizi ya msimu.

Timu hizo zenye hadhi kubwa Afrika mashariki na kati kiasi cha kuwa kivutio kikubwa katika michuano hiyo zote zina mpango wa kuweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya nje ya nchi na tayari zimepanga kuwarejesha mastaa wake mwanzoni mwa mwezi Julai tayari kwa maandalizi.

Michuano ya Cecafa Kagame Cup yamerudi mwaka huu baada ya kutofanyika kwa miaka kadhaa lakini changamoto kubwa ni ratiba kuwa ngumu kwa vilabu kadhaa katika ukanda wa Cecafa kutokana na kubanwa na ratiba za maandalizi ya msimu mpya na hatua za awali za michuano ya Kimataifa ambayo inatarajiwa kuanza mwezi Augusti.

Pamoja na kwamba Simba sc na Azam Fc mpaka sasa haijajulikana zitaweka kambi nchi,Kwa upande wa Yanga sc inatajwa kuweka kambi katika Urusi ama Afrika ya kusini ambapo pia ina mialiko ya kucheza michezo ya kirafiki na klabu za Cska Moscow na Kaizer Chiefs.

Azam Fc tayari imeshatoa taarifa rasmi kupitia kwa meneja wa idara yake ya Habari Zakaria Thabit kuwa haitoshiriki michuano hiyo huku Simba Sc na Yanga Sc zikiwa bado mpaka sasa hazijatoa taarifa rasmi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala