Connect with us

Soka

Singida Fg Yauza Mastaa Kulipa Madeni

Klabu ya Singida Big Star imeamua kuwauza baadhi ya nyota wa klabu hiyo ili kukusanya kiasi cha fedha kwa ajili ya kulipa madeni yanayoikabili klabu hiyo kiasi cha kufungiwa na Shirikisho la soka duniani (Fifa) kufanya usajili.

Maamuzi hayo yametangazwa mchana wa leo na Mtendaji mkuu wa klabu hiyo Japhet Makao wakati akiongea na waandishi wa habari kufafanua mambo kadhaa hasa baada ya taarifa kusambaa kuwa baadhi ya mastaa wameuzwa katika timu ya Ihefu Fc.

“Tumeamua kuwaweka sokoni wachezaji kadhaa ili tumalizane na Fifa” Rais wa Singida Fountain Gate FC, Japhet Makau akifafanua taarifa mbalimbali zilizozuka mitandaoni ikiwemo ile ya kuuzwa kwa wachezaji wa kikosi hicho katika Timu ya Ihefu SC.

Mastaa kama Gadiel Michael tayari amepata timu nchini Afrika ya Kusini ya Cape Towns Spurs ambayo atajiunga kwa mkataba wa mwaka mmoja huku Mouruf Tchakei,Khomein Abubakar,Joash Onyango na Duke Abuya wamejiunga na Ihefu Fc.

Makau amesisitiza kuwa lengo la kufanya hivyo ni kupunguza matumizi pamoja na kupata fedha za kulipa madeni ya wachezaji wanaoidai klabu hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka