Connect with us

Soka

Singida FG Waanza Usajili

Klabu ya Singida Fountain Gates imekamikisha Usajili wa Mlinzi wa kushoto raia wa Botswana Benson Kitso Mangolo kuja kuongeza nguvu katika eneo hilo ambalo mpaka sasa anacheza Gadiel Michael na Yahaya Mbegu kikosini humo.

Benson ambaye amewahi kuwa mchezaji bora wa mwaka nchini Botswana, kabla ya kukamisha usajili wake na matajiri wa Alizeti wenye makazi yao mkoani Singida huku ikifahamika kuwa Benson alikuwa ameshaitumikia klabu ya Jwaneng Galaxy inayoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika,

Usajili umefanikishwa kwa kiasi kikubwa na  Olebile Sikwane ambaye ni Mtendaji mkuu (CEO) wa klabu hiyo ya Singida ambapo kutokana na kufanya kazi nchini humo ilikua rahisi kwake kukamilisha Usajili huo haraka zaidi,

Singida FG katika usajili huo wameishinda Changamoto kutoka Kwa baadhi ya Vilabu kutoka Afrika Kusini ikiwemo Amazulu Fc ambayo ilikua ikimnyemelea kwa ukaribu zaidi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka