Connect with us

Makala

Singida Black Stars Yailiza Dodoma Jiji

Klabu ya soka ya Singida Black Stars imefanikiwa kupata alama tatu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma jiji katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Ccm Liti mkoani Singida.

Mabao mawili ya haraka haraka ya Elvis Rupia dakika ya 8 na 15 yalitosha kuwapa alama tatu muhimu wenyeji hao huku Dodoma Jiji wakijitahidi kusawazisha bila mafanikio yeyote.

Katika mchezo huo Singida Black Stars iliutawala kuanzia mwanzo mpaka mwisho huku kukosa umakini kwa washambuliaji wake kulisababisha wasipate ushindi mnono.

Sasa Singida Black Stars imefanikiwa kuzishusha Simba sc na Yanga sc baada ya kufikisha alama 30 katika nafasi ya pili ya ligi kuu ya Nbc nchini ikiwa imecheza jumla ya michezo 14 ya ligi kuu nchini.

Hata hivyo Singida Black Stars inatakua na wakati mgumu siku ya Disemba 28 itakapovaana na Simba sc katika uwanja wa Ccm Liti mchezo ambao utakua na maana kubwa endapo itaibuka na ushindi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala