Connect with us

Soka

Simba yawachezesha makhirikiri Jwaneng

Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Bara na wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya kombe la ligi ya mabingwa Barani Afrika Simba Sc imewachakaza mabingwa wa Botswana Jwaneng Galaxy kwa mabao 2-0 ugenini katika dimba la Taifa la nchi hiyo Jijini Gaborone.

Simba walijipatia magoli yake yote mawili katika dakika ya tano za kipindi cha kwanza,mkata umeme Tadeo Lwanga ndiye alikua wa kwanza kuiandikia timu yake bao kwa shuti kali dakika ya pili akitumia vema makosa ya golikipa wa Jwaneng.Wakati Jwaneng wakijiuliza nahodha John Bocco aliwanyanyua tena Simba kwa shuti kali ndani ya kumi na nane dakia ya tano.

Simba itarudiana na Wabotswana hao Oktoba 24 mwaka huu Jijini Dar es salaam wakiwa na mtaji mzuri wa magoli ya ugenini.

Endapo wakishinda mchezo huo au kupata sare watafuzu moja kwa moja kwenye makundi ya michuano hiyo,huku Jwaneng wakishuka katika michuano ya kombe la shirikisho kusaka tiketi ya makundi ya michuano hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka