Connect with us

Soka

Simba Sc Yazindua Jezi Kalii

Klabu ya Simba sc imeanza kampeni kuelekea michezo ya ligi ya mabingwa hatua ya makundi baada ya kuzindua jezi mpya kwa ajili ya kuanza kuzitumia katika michuano hiyo ambapo wataifungua siku ya jumamosi watakapokutana na Asec Mimosa ya nchini Ivory Coast.

Jezi hizo ziko aina tatu za nyumbani,Ugeni na jezi ya tatu ambayo ina rangi ya Blue huku zile zingine zikiwa na rangi nyekundu na nyeupe.

Katika uzinduzi wa jezi hizo mastaa kama Moses Phiri,Che Malone Fondoh,Abdalah Hamis na David Kameta wametumika kunogesha muonekano wa jezi hizo.

Jezi hizo zimedizainiwa na mzalishaji na msambazaji wa jezi za klabu hiyo kampuni ya Sunderland the only one na tayari zimeanza kupatikana katika maduka ya mzalishaji huyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka