Connect with us

Soka

Simba Sc Yaweka Rekodi Afrika

Klabu ya Simba sc imefuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika ikifanikiwa kufuzu kwa kufunga idadi kubwa ya mabao katika mchezo baada ya kuifunga timu ya Janweng Galaxy ya Botswana 6-0 katika mchezo uliofanyika siku ya Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Simba sc iliwalazimu kushinda mchezo huo ili kukata tiketi kutokana na kuwa na alama sita katika kundi B huku Wydad Ac wakiwa na alama sita pia ambapo walikua wanaivizia nafasi hiyo ya kufuzu kundi B kama washindi wa pili baada ya Asec Mimosa kufuzu kama kinara wa kundi.

Simba sc ilifanikiwa kufunga bao la kwanza lililowapunguzia presha ya mchezo likifungwa na Saido Ntibanzokiza alipokea pasi nzuri ya Cletous Chama dakika ya 7 ya mchezo huku Pa Omari Jobe akifunga bao la pili dakika ya 14 na Kibu Dennis akifunga ba0 la tatu dakika ya 22 na kuufanya mchezo kwenda mapumziko Simba sc wakiwa mbele kwa mabao 3-0.

Kipindi cha pili Janweng walianza kwa nidhamu ya kuzuia lakini walijisahau dakika ya 76 ya mchezo ambapo Chama alifunga bao la nne na dakika kumi baadae mabeki wa Janweng walijisahau kuokoa mpira wa kona na kumkuta Fabrice Ngoma aliyefunga akiwa hajakabwa.

Kocha Benchika ambaye alimuingiza Ladack Chasambi mwishoni mwa mchezo alifanikiwa kuchanga karata yake vyema na kufunga bao la sita kwa Simba sc akimalizia krosi iliyopigwa na Fredy Michael Koublan ambaye aliwachambua mabeki wa Galaxy na kutoa pasi kwa mfungaji.

Kufuzu kwa Simba sc kunaingia katika rekodi za timu zilizofunga mabao mengi katika michuano hiyo hatua ya makundi ambapo pia waliwahi kumfunga Horoya Fc idadi ya mabao 7-0 katika mchezo pia wakiifanya Tanzania kuwa taifa pekee lililopeleka timu mbili katika michuano hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka