Connect with us

Soka

Simba sc Yawasili Ivory Coast

Kikosi cha klabu ya Simba sc tayari kimewasili nchini Ivory Coast kuelekea mchezo wa tano wa hatua ya makundi dhidi ya Asec Mimosas utakofanyika siku ya ijumaa nchini humo ambapo timu hizo zipo katika kundi B la michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

Kikosi hicho kimewasili nchini humo kikiwakosa mastaa wake John Bocco,Willy Onana na Ayoub Lakred ambao ni majeruhi huku mastaa wa kikosi cha kwanza wengine wakiwa wamesafiri na timu akiwemo Henock Inonga ambaye alikua katika michuano ya mataifa ya Afrika na timu ya Dr Congo na kukosa michezo ya mwanzo ya klabu yake.

Simba sc ikiwa na alama tano inapaswa kushinda mchezo huo ili kufikisha alama nane kabla ya kuwakaribisha Janweng Galaxy hapa nchini ambapo wakishinda basi moja kwa moja watapata tiketi ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya klabu barani Afrika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka